Habari

CAG Prof. Assad “Nitaitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka”

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Prof Mussa Asad amekiri kuwa ataitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka ya Bunge January 21 2019, Prof Asad amepokea wito rasmi wa maandishi January 15 2019

Prof Assad ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki chache toka Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka mkaguzi huyo kwenda kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka ya Bunge kwaajili ya kuhojiwa kufutia kauli yake ambayo ilitafsiwa kwamba amesema Bunge ni dhaifu.

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Bunge ni Taasisi ambazo lazima zielewane na kufanya kazi kwa karibu sana, kwa imani yangu nina mahusiano mazuri na Bungeā€, CAG Prof. Mussa Assad

Aliongeza, “Majibu yangu katika mahojiano yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge hata kidogo, maneno kama udhaifu ni lugha ya kawaida sana kwa Wakaguzi kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali”

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge, Job Ndugai amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana mambo mbalimbali yanayozungumzwa mtandaoni likiwemo la CAG.

“Sisi Tanzania tumeweka Balozi nchi mbalimbali na maofsa ambao kazi yao ni kui-brand nchi yetu, hizo ni gharama. Marekani wanatupa misaada halafu wewe ofisa unatoka Tanzania unaenda kule unasema Bunge la Tanzania ni ‘Bogus’,” alisema Spika wa Bunge, Job Nduga

Aliongeza “Nasema Bunge siyo dhaifu, walisema Serikali ya Awamu ya Nne, kwani nyie hamukuwepo kwamba Serikai ile ni dhaifu. Sasa hivi wanasema tena, wengine wapo Segerea, wanarudia kusema serikali ni dhaifu? Wanakimbia kwa Ndugai wanafikiri kule ndo rahisi zaidi.,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents