Habari

CCM yawataka waliotajwa kwenye sakata la Madini kutoa ushirikiano

Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, amesema CCM inampongeza Rais Magufuli (Mwenyekiti wa CCM) kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia rasilimali za Taifa.

“Watu waliotajwa kwenye taarifa zote mbili na hasa kwenye hii ya Profesa Osoro, Rais ameelekeza vyombo vyote vinavyohusika viwahoji watu hawa. Mimi nitoe msisitizo kama chama chenye serikali watu hawa watoe ushirikiano unaostahili, watusaidie kujua nini ni nini na nani ni nani na ilikuaje alafu tutaujua ukweli,” alisema Polepole.

“Uamuzi umefanyika siku mbili zilizopita na utakapo kuwa tayari utatusaidia na sisi kama chama kutafakari tunataka zoezi hili liende kidogokwa haraka ili tuone Watanzania wananufaika na rasilimali hizi kilicho cha haki kwa Watanzania kipatikane.”

Hata hivyo Polepole, amesema kilichofanywa na Rais Magufuli ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya wawekezaji katika migodi ya Madini nchini.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents