Habari

CEO wa Snapchat aeleza kwanini alikataa ofa ya Facebook kuinunua app yake kwa dola bilioni 3

Snapchat iliishangaza Jumuiya ya teknolojia mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kuripotiwa na Wall Street Journal kuwa ilikataa ofa kutoka kwa Facebook ya kuiuza app hiyo kwa dola bilioni 3.

Snapchat-CEO-Evan-Spiegel

Akiongea na Forbes kuhusu sababu za kutoa mkwanja huo mnene, CEO wa Snapchat, Evan Spiegel alisema: Kuna watu wachache duniani wanaoweza kutengeneza biashara kama hivi. Nahisi kuiuza kwa faida ya muda mfupi si kitu cha kuvutia sana.”

Mwanzilishi na CEO wa Facebook, Mark Zuckerberg alimfuata Spiegel kwenye mji anaoishi mwaka jana na kuwaambia waanzilishi Snapchat kuwa Facebook imepanga kuzindua app inayofanana na yao. “Kimsingi ilikuwa kama ‘tunakuja kukumaliza,'” Spiegel aliliambia jarida la Forbes kuhusu mkutano hup. App hiyo ilikuwa Facebook Poke, ambayo hata hivyo imeangukia pua.

Zuckerberg aliwafuata kwa mara ya pili kusisitiza dau lake lakini waanzilishi hao wa Snapchat wakamtosa tena. Kwa sasa Snapchat inathaminiwa kwa dola bilioni 2, chini ya dau walilopewa na Facebook.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents