Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Chege ataja sababu ya kukosekana hits song nyingi

Msanii kutoka TMK Wanaume, Chege Chigunda ameeleza kwa sasa kuna vita ya muziki kwa Tanzania hivyo kupelekea kukosekana kwa hits song nyingi.

Akipiga stori na Times Fm katika kipindi cha Twenzetu ambapo aliulizwa kwanini hamna hit song kubwa tangu mwaka jana ilipotoka ya Darasa ‘Muziki’.

“Unajua kuna mabadiliko ya muziki, ukiangali Marekani nako ni hivyo hivyo, ukiangalia Nigeria ni hivyo hivyo… zamani ulikuwa akisikia ngoma imetoka Fall in love inakuwa Fall in love dunia nzima umeona ukisikia Do Me, basi dunia nzima lakini sasa kilichotokea Nigeria ndicho kinatokea sasa sio kwamba watu hawapigi mziki mkali, kuna vita ya muziki inafanyika,” amesema Chege.

Pia mkali huyo ameongeza kuwa ” Zamani ilikuwa unaona singo moja inatoka kwa mwezi ya msanii mmoja au unakuta singo mbili zinatoka, lakini sasa kwa siku zinatoka karibu singo saba hiyo ndio sababu.”

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW