Shinda na SIM Account

Chid Benz: Ni kweli nilikamatwa ila si madawa

Rapa kutoka kundi la LaFamila, Chid Benz ametoa ufafanuzi wa kukamatwa kwake siku ya Agosti 12 mwaka huu baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.

Chid amekanusha vikali tuhuma hizo kupitia E-Newz ya EATV na kusema kuwa stori hizo zinatengenezwa na washindani wake ili kumharibia kimuziki.

“Mimi nimekamatwa kweli lakini sikukamatwa na madawa na wala si kukutwa navuta madawa na pia nimefanya vipimo na sijakutwa na madawa. Kama unavyojua kuna kitu kimoja watu wanachanganya unakuta mtu anasema aah yule kesha zidi bhana, watu wengi wanaomsaidia sasa hivi wameshakufa nguvu unamsaidia hivi ana haribu tena,’ amesema Chid.

Pia akaongeza kuwa “Watu wasitengeneze stori zangu ziwe ni kitu kibaya katika muziki wangu, watu wangu wale wabaya ni washindani wangu wanachukua stori zangu na kuzifanya zisambae vibaya, lakini kama watu wanaelewa huu ni ushindani yani watu wanamuogopa sana Chid kwa hiyo inapotokea habari yoyote mbaya ndiyo inakuwa advantage wanachukua habari mbovu inatengenezwa inasambazwa.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW