BurudaniUncategorized

Clouds Media watangaza ujio mpya wa Fiesta 2018, ni shavu la wasanii wa ndani kwa 100%

Kampuni ya Clouds Media Group Jumanne hii imetangaza ujio mpya wa Tamasha kubwa la muziki la Fiesta baada ya kusubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa burudani nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Tamasha hilo ndani ya mwaka huu limekuja na kauli ‘VibeKamaLoteeeeee’. Lakini bado hawajaanza kutangaza list ya wasanii ambao watashiriki.

Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo, William Mpinga ameeleza kwamba Tigo Fiesta 2018 itaendeleza utamaduni wa ‘100% Local’ (yaani wasanii wa ndani kwa asilimia 100).

 

“Tangu Tigo iingie kwenye tamasha hili, uwezo wa wasanii wetu wa ndani umeongezeka. Mwaka jana tumewaona wakifanya ‘live perfomance’ katika viwango vya kimataifa na hivyo tumejiridhisha kwamba wao wanatosha kutoa VibeKamaLoteeee bila kutegemea wasanii wa nje”

Hata hivyo mwaka huu ni tofauti na miaka mingine kwani tamasha hilo lilikuwa linaanza mapema zaidi na kumalizika mwezi October au November.

Pia kampuni hiyo kongwe katika masuala ya burudani nchini haijaweka wazi safari hii litazunguka katika mikoa mingapi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents