Burudani

Cpwaa kuwa msemaji kwenye mjadala kuhusu mchango wa ICT kwenye tasnia ya burudani nchini

Rapper Ilunga Khalifa aka Cpwaa anatarajia kuwa msemaji kwenye kongamano litakaloangalia mchango wa teknolojia ya habari na mawasiliano ICT katika tasnia ya burudani nchini.

BEwDjJICAAED3GP.jpg large

Pamoja na kuwa mwanamuziki, Cpwaa ni msomi wa IT.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika March 11 katika ofisi za KINU zilizopo mitaa ya Morocco, barabara ya Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Wazungumzaji wengi kwenye kongamano hilo watakuwa pamoja na Rashid Shamte (Head of Group Strategy Six Telecoms)na Luca Neghesti (Entrepreneur, Founder of Bongo5 and Co-founder of KINU).

Wengine ni Charles Matodane (Head of Value Added Services (VAS) & Internet at Vodacom) na Hussein Mkwazi (mwanafunzi wa mwaka wa mwisho IFM / part-time programer(ametengeneza Bao game).

Kongamano hilo litafanyika kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku. Ili kushiriki fuata link hii ujiandikishe

http://momodarmusic.eventbrite.com/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents