Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Dayna Nyange: Sikupanga kuitoa ‘Pepea’

Dayna Nyange amedai kuwa wimbo wake uliotoka hivi karibuni ‘Pepea’ umevuja na kwamba hakuwa amepanga kuutoa.

10724128_1495740010704857_627078543_n

“Yaani nimepokea simu nyingi sana kuhusu huu wimbo mpya unaitwa Pepea nikabaki nashangaa tu maana huo wimbo nilifanya siku nyingi hata kabla sijatoa wimbo wa I Do,” ameiambia Bongo5.

“Naomba niwaambie tu mashabiki wangu kuwa huo wimbo sijautoa rasmi na nilikuwa sijapanga kuutoa sasa hivi kabisa, nilipanga kutoa wimbo wangu mpya mwezi huu mwishoni. Sijapenda kabisa na sijui ni nani ametoa huu wimbo. Niliufanya C9 Records, na mimi huwa sipendi kuwa navujisha nyimbo zangu. Kama mtu unajiamini unaweza hauwezi kuvujisha nyimbo. Bado sijajua hadi sasa hivi itakuaje, naongea bado na team yangu ili tujue tunafanyaje.”

Usikilize wimbo huo hapo chini.

Related Articles

Leave a Reply

Check Also

Close
Bongo5

FREE
VIEW