Burudani

D’banj kupata mtoto wake wa kwanza?

Msanii wa muziki kutoka Nigeria ,Oladapo Daniel Oyebanjo maarufu kama D’banj anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mkewe, Lineo Didi Kilgrow kwa mujibu wa mitandao ya Nigeria.

D’banj mwenye miaka 36 na mkewe mwenye miaka 26 walifunga ndoa ya siri, Julai 2016 jijini Lagos, Ndoa ambayo iliudhuriwa na ndugu pekee.

Banj ndiye aliyetangaza taarifa za kupata mtoto na mkewe. Mtoto huyo ndio wa kwanza kwa msanii huyo tangu afunge ndoa.

Lineo ambaye yupo nchini Marekani atakuwa huko akisubiria kujifungua.

Licha ya muziki pia D’banj anajihusisha na biashara pamoja na utangazaji wa kipindi cha TV.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents