Habari

DC Jerry Muro aanza kazi kwa kasi, akamata Malori 10 kutoka Kenya ‘hii ndio kazi niliyotumwa’ (+video)

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amefanya zoezi la ukaguzi wa malori 10 yaliyokuwa yakitokea Nchi jirani ya Kenya.

Mara baada ya kuyatilia mashaka Malori hayo kutoka Mombasa kupitia njia ya Namanga tukio ambalo limeonekana sio la kawaida Kwa magari hayo kupitia njia ndefu ya Namanga kutoka Mombasa kwenda Dar es salaam.

DC Muro akiwa katika majukumu yake Siku ya Jumapili Jioni alishangazwa na kitendo cha Malori hayo mapya kupita katika Wilaya yake kwa kutumia boda ya Namanga badala ya kupitia Tanga mida ya jioni yakiwa na *chesses number* ambazo alizitilia mashaka.

Muro amesema amewaagiza Maofisa TRA kuyagua Malori hayo ili kujiridhisha kutokana na kuwepo Kwa tetesi za baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuhujumu Bandari za Tanzania na kukimbilia Nchi Jirani kutokana na Bandari za Tanzania kuwa na udhibiti mzuri wa Vitendo vya Magendo na Rushwa .

DC Muro ameahidi kuwa katika Wilaya anayoiongoza ya Arumeru Kamwe haitakuwa uchochoro wa kupitisha bidhaa haramu za magendo kutoka Nchi Jirani.

Related Articles

6 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents