DC Jokate ageuka mbogo kijiji kugeuka kijiwe cha umbea na majungu (Video)

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo amewataka wakazi wa Kijiji cha Masaki Kisarawe kuacha majungu na umbea kwani tabia hiyo imekifanya kijiji hicho kishindwe kuendelea kwa muda mrefu.

Ameyasema hayo Ijumaa hii alivyotembelea Kijijini hapo kwaajili kuona mradi wa akina Mama 25 Wajasiriamali ambao aliwatafutia tsh milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa Mgahawa wakisasa ambao utaingizia pesa na kuwainua kichumi.

Alisema moja ya changamoto ambazo zinakisumbua kijiji hicho ni tifina na umbea hali ambao amedai umekirudisha nyuma kijiji hicho kimaendeleo.

Nao Wanakijiji wa eneo hilo wakiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kumuahidi Mkuu wa huyo wa Wilaya kwenda kuifanyia kazi huku akimshukuru kwa kuiongea kero hiyo hadharani.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW