Tupo Nawe

Dhamana ya Ronaldinho kutoka jela akiwa na kaka yake ni kufuru, Watakiwa kukaa hotelini kwa uangalizi maalumu – Video

Dhamana ya Ronaldinho kutoka jela akiwa na kaka yake ni kufuru, Watakiwa kukaa hotelini kwa uangalizi maalumu - Video

Taarifa ambayo hii imetolewa na Jaji wa kesi ya Ronaldinho ambae anafahamika kama Gustavo Amarila zinasema kwamba Staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho na kaka yake Assis wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32.


Ronaldinho na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka.

Pamoja na kupata dhamana hiyo lakini jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum.

Ronaldinho na Assis walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport bandia za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil.

View this post on Instagram

Dhamana ya Ronaldinho kutoka jela akiwa na kaka yake ni kufuru, Watakiwa kukaa hotelini kwa uangalizi maalumu Taarifa ambayo hii imetolewa na Jaji wa kesi ya Ronaldinho ambae anafahamika kama Gustavo Amarila zinasema kwamba Staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho na kaka yake Assis wamepata dhamana na kutoka gerezani nchini Paraguay baada ya kukaa huko kwa siku 32. Ronaldinho na Kaka yake wamepata dhamana kwa dola milioni 1.6 (Tsh Bilioni 3.7) baada ya awali kukataliwa dhamana nyepesi kwa hofu wangeweza kutoroka. Pamoja na kupata dhamana hiyo lakini jaji Gustavo Amarilla ameamuru wawili hao kutolewa gerezani na kwenda kuishi katika nyumba/hotel katika mji wa Asuncion wakiwa chini ya uangalizi maalum. Ronaldinho na Assis walikamatwa na Polisi nchini Paraguay kwa tuhuma za kuingia nchini humo na Passport bandia za Paraguay ambazo zinawaonesha wao kama raia wa nchi hiyo wakati ni raia wa Brazil. Written and edited by @el_mandle

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW