Aisee DSTV!

Diamond ala sahani moja na Chris Brown kwenye mtandao wa YouTube, Tanzania aweka rekodi mpya

Kwasasa Tanzania ukitaja video ya muziki iliyotazamwa zaidi ndani ya muda mfupi, Basi wimbo wa Kanyaga wa Diamond Platnumz ndio wimbo ulioweka rekodi hiyo mpya kwa kutazamwa mara milioni 1 “views milioni 1” ndani ya masaa 13.

Wimbo huo unakuwa wa kwanza baada ya kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na video ya wimbo wa Hallelujah iliyowahi kutazamwa mara milioni 1 ndani ya masaa 15.

Wimbo mwingine ambao nao ni moja ya nyimbo tatu zilizofikisha views milioni moja kwa muda mfupi ni Inama, Ambao Diamond Platnumz amemshirikisha Fally Ipupa kutoka DR Congo.

Wimbo huo ulitazamwa mara milioni 1 ndani ya masaa 16 tangu uwekwe kwenye mtandao wa YouTube.

Hiyo orodha ni ya nyimbo tatu hapa Tanzania, ambazo zimefikisha views milioni moja kwa muda mfupi zaidi tangu ziwekwe kwenye mtandao wa YouTube.

Wakati hayo yakijiri hapa Tanzania, Kule nako Marekani msanii wa muziki, Chris Brown aliachia wimbo wake mpya wa Don’t Check On Me ambao nao mpaka kufikia masaa 12 ulikuwa umeshasikilizwa mara milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW