Burudani ya Michezo Live

Diamond awaomba Watanzania hili kuhusu Samatta, Mbosso amuunga mkono “Akihama timu nahama nae” – Video

Diamond awaomba Watanzania hili kuhusu Samatta, Mbosso amuunga mkono "Akihama timu nahama nae"

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na C.E.O wa lebo kubwa ya muziki ya WCB na Wasafi Media Diamond Platnumz ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza Mtanzania Mbwana Ally Samatta baada ya kujiunga na klabu ya Aston Villa akitokea KR Genk.

Diamond akiwa na shabiki mkubwa wa Samatta amewaomba Watanzania kumsapoti Samatta na kusema kuwa amehama kwenye timu anayoipenda ila popote Samatta aendapo na yeye humfuata.

Ujumbe wa Diamond unasomeka hivi:-

“Nlichokifanya ni kuhama kwenye team yangu na Kuhamia @avfcofficial , na akihama tena team nyingine nahama nae…..najua pengine una team uipiendayo ila ombi langi ukishindwa kuhamia kama Mie, walau iwe team yako ya pili ili tuzidi kumpa Nguvu @samagoal77 CHAMP!!!…..🌍🏆🌍 #HiiNiTanzaniaMpya”

Mbali na hilo kwenye hiyo post ya Diamond msanii wa lebo yake Mbosso nae hakuwa mbali aliandika maneno haya:-

Nipo @simbasctanzania na @chelseafc .. ila Sasa nimejisogeza @avfcofficial Kwa Mkataba wa Miaka 4 na nusu .. @samagoal77

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW