Habari

Mamalaka ya hali ya hewa Tanzania ‘TMA’ yatoa tahadhari mikoa 5 kukumbwa na mvua na upepo mkali kwa siku tano – Video

Mamalaka ya hali ya hewa Tanzania 'TMA' yatoa tahadhari mikoa 5 kukumbwa na mvua na upepo mkali kwa siku tano - Video

Mamalaka ya hali ya hewa nchini  (TMA), imetoa tahadhari ya uwezekano wa uwepo wa mvua kubwa kwa Mikoa mitano nchini Tanzania, ikiwemo Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mvua hizo zitanyesha kuanzia Januari 21 hadi Januari 25, 2020.

“Tunatoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa kwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara, athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa shughuli za uvuvi, ucheleweshwaji wa usafiri pamoja na kuanguka kwa majani na matawi madogomadogo ya miti.” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha mamlaka hiyo imewataka wananchi wa Mikoa hiyo, kuzingatia tahadhari iliyotolewa na wajiandae.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents