Diego Maradona aipa ofa timu ya taifa ya Argentina ‘naumia kuona timu yangu inapotea’

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Diego Maradona amesema kuwa uvumilivu umemshinda kuona timu yake ya taifa ikikosa mataji makubwa duniani na kuamua kujitolea kukinoa kikosi hicho bila malipo.

Image result for maradona
Diego Maradona

Maradona ambaye ameshinda kombe la dunia la mwaka 1986 na timu ya taifa ya Argentina amesema kuwa nafasi ya Sampaoli kusalia kama kocha wa timu hiyo ni ndogo sana kufuatia kuvurunda kwenye kombe la dunia.

Namuomba japo Mungu anipe nguvu niwe na nguvu kama zamani kwani naumia kuona timu yangu inapotea kirahisi rahisi, mbaya zaidi naumia kuona timu yangu inakuwa mbovu hata kwenye michuano yenye timu 32 hii ni aibu kubwa kwa timu tuliyotumia nguvu kubwa na miaka mingi kuijenga, nitarudi kuifundisha timu yangu tena bila hata malipo. Hebu fikiria nimekimbia umbali gani nikiwa na jezi na bendera ya taifa langu? narudi kuifundisha timu yangu siwezi kukubali matokeo tuliyoyapata,“amesema Maradona kwenye mahojiano na ESPN.

Hata hivyo, Kocha huyo hataweza kufukuzwa kiurahisi na chama cha mpira nchini Argentina (AFA) kwani atatakiwa kulipwa kiasi cha dola milioni $17.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW