Habari

Dkt Kikwete asaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Dkt. Mwakyembe

By  | 

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesaini kitabu cha maombolezo kwenye msiba Linah George Mwakyembe, ambaye ni mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

Kikwete amewasili msibani hapo leo mchana na kuweka saini kwenye kitabu hicho.

Waliofika kumfariji Dkt Mwakyembe Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete,Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja,Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Benard Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje,.

Kifo cha Mke wa Dkt Mwakyembe kilitokea Jumamosi katika hospitali ya Agha khan alipokuwa akipatiwa matibabu.

Na Emmy Mwaipopo

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments