Habari

Dkt Mpango akifungia kituo cha mafuta cha GBP

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameamuru kituo cha Mafuta cha GBP kifungwe hadi hapo kitakapo funga mashine maalum za kutolea risiti(EFD) baada ya kubainika hakitumii ipasanyo mashine za kieletroniki.

Dkt Mpango alifanya ziara ya kushitukiza katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuamuru kituo hicho cha mafuta kufungwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya kujionea kituo hicho kilkuwa na pampu nne za mafuta lakini kuna mashine moja pekee ya mkononi ya kutolea risiti jambo linasababisha wateja wao wengi kutopewa risiti hivyo kuipelekea serikali kukosa mapato.

“Sasa nawachukulia hatua ili liwe fundisho kwa wengine wote wanaouza mafuta nchini bila kufuata taratibu, na nitaanza na wewe, biashara yako isimame mpaka mashine zifungwe kwenye kituo chote na utekeleze mara moja,” alisisitiza Dkt. Mpango.

Katika hatua nyingine Dkt Mpango ameiagiza Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini wamiliki wa vituo vya mafuta wanaokiuka maagizo ya serikali yaliyowataka wafunge mashine hizo maalum.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents