Burudani

Dr. Dre aomba radhi kwa ukatili aliowafanyia wanawake

Dr. Dre ameomba radhi kwa ukatili aliowahi kuwafanyia wanawake miaka mingi iliyopita.

Dr.-Dre

Rapper na producer huyo ameandika maelezo yake kupitia gazeti la The New York Times na kudai kuwa amebadilika.

“Miaka 25 iliyopita nilikuwa kijana mdogo ninayekunywa sana pombe kichwani mwangu sikuwa na mpangilio wa maisha,” alisema.

“Hata hivyo, yote haya si sababu ya kukwepa niliyofanya. Nimeoa kwa miaka 19 na kila siku najitahidi kuwa mwanaume bora kwa familia yangu, nikitafuta muongozo njiani. Nafanya kila kitu ninachoweza ili nisifanane na mtu huyo tena.”

“Ninawaomba radhi wanawake niliowaumiza. Ninajuta sana kwa kile nilichokifanya na najua kuwa kimeathiri maisha yetu.”

Nayo kampuni ya Apple, ambayo Dre anafanya kazi kama mmoja wa washauri wakuu imetoa maelezo yake;

Dre has apologized for the mistakes he’s made in the past and he’s said that he’s not the same person that he was 25 years ago. We believe his sincerity and after working with him for a year and a half, we have every reason to believe that he has changed.”

Wanawake hao ambao Dre aliwapiga katika miaka ya 90 ni pamoja na Dee Barnes na Michel’le.

Michel’le, aliyezaa mtoto wa kiume na Dre mwaka 1991, anadai kuwa kipigo hicho kilimpa macho meusi, kuvunjwa mbavu na makovu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents