Habari

Dr3am Ville kundi la Hip Hop la Kenya linalowapa moyo vijana kutozikatia tamaa ndoto zao

Dr3am Ville (inasomeka Dreamville) ni kundi la hip hop la Kenya lililoanzishwa January 14, 2012. Linajumuisha wasanii watatu ambao ni pamoja na Mishu, Webb, na R.H.

Dream ville

b693acc1-9200-49ab-92f8-77cb40db7cf8

Wasanii waliowashawishi members wa kundi hili kuingia kwenye muziki ni pamoja na K’Naan, Sade, P-Square, Sauti Sol, Juliani, Sway De Safo, Spoek Mathambo, Toya DeLazy, TearGas na wakongwe kama Bob Marley, Tupac na Michael Jackson.

Mwaka 2012, walitoa mixtape yao ya ushirikiano, Wild in the Ville. Katika mixtape hiyo waliwashirikisha wasanii kutoka Zambia (Urban Hype & Krytic), South Africa (ProdaJae), Jamaica (GBanks), Bangladesh (R.Smug), India(Phenomenal), Ujerumani (Araxx) na Marekani (Kast One, Crow & Ronmixa).

Pamoja na kuwa na uhusiano mzuri na wasanii wenzao, mixtape hiyo iliwapa mashavu zaidi ambapo single yao Breakthru, ilijumuishwa kwenye mradi unaodhaminiwa na World Hip Hop Market katika mixtape ya AHHM vol. 3.

Nyimbo zao pia zilipata airplay kwenye vituo vikubwa vya radio katika nchi mbalimbali kama Botswana (Yarona FM), Zimbabwe (Zi FM), Malawi (Radio 2 FM) na radio za mtandaoni za Marekani kama Phenom Radio (Texas) na Top Fm, ya Uingereza.

Mpaka sasa Dream Ville wameshapanda jukwaani na wasanii kama Jua Cali, Madtraxx, Elani, Mejja na wengine wa Kenya. Nyimbo zao nyingi zimekuwa zikiwapa moyo vijana kutokataa tamaa, kuwa wavumilivu na kuendelea kupambana wafanikiwe kwenye ndoto zao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents