Burudani

Drama: Jay-Z akanusha uvumi kuwa mkewe Beyonce ni mjamzito!

Kumekuwepo na taarifa kuwa huenda Beyonce na Jay Z wanategemea kumletea binti yao kipenzi Blue Ivy mdogo wake kutokana na Beyonce kuwa mjamzito kama ilivyoripotiwa na vyombo vingi vya habari duniani,

jay-z-beyonce-island

Hata hivyo zimejitokeza taarifa zingine zinazosema kuwa Jay-Z amekanusha uvumi huo na kusema kuwa taarifa hizo sio za kweli. Kwa mujibu wa kituo cha radio cha Hot 97 huko New York, jana mtangazaji wa kituo hicho aitwaye Ebro akiwa hewani alithibitisha kuwa amepokea email kutoka kwa Hov mwenyewe ambayo inakanusha uvumi huo na kunukuu baadhi ya maneno yaliyo katika email hiyo “It’s not true. The news is worse than blogs.”

Ebro pia ni station manager wa kituo cha Hot 97 na amekuwa na ukaribu na Jay kwa kipindi kirefu, hivyo inawezekana kweli amepokea email ya Jigga lakini kuna uwezekano pia mtu mwingine akawa ameamua kutuma email hiyo akijifanya ni Jay. Let’s wait.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents