Habari

Dudu Baya: Stress za game zinawasababisha wasanii kunywa pombe kuvuta bangi na baadaye kubwia unga

Msanii mkongwe wa Hip Hop na mjasiriamali, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amesema stress za muziki zinawaumiza wasanii wengi na kuwafanya wanywe pombe, wavute bangi na baadaye kuzama kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Dudu-Baya

Dudu Baya ambaye hivi karibuni aliachia wimbo mpya, Power of Jesus unaoelezea hali ya maisha, ametoa ushauri kwa wasanii wenzie kuwa wasikate tamaa bali wajipange na kuangalia wamekosea wapi.

“Mimi sina stress na game, kwanza mimi nina jina kubwa sana nina makampuni ya mbao Mambas Timber, huko mwanza, Mambas Entertainment na hii Mambas Pub nasonga mbele na maisha. Kwahiyo ningekuwa na stress ningekuwa kama hawa wasanii wenye stress ambao wanakunywa pombe, bangi na mwishowe wanakula madawa, unatakiwa uongee na Mungu akupe matumaini,” ameiambia Bongo5.

Amesema pia kuwa yeye ni professional kwenye uchoraji ramani za majengo na fundi.

“Nimejenga majumba mengi kwhaiyo nafanya mengi naweza kuwaajili baadhi ya wasanii ambao wamechoka na maisha.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents