Burudani

Picha: Kafulila na Zitto waungana na EFM kusherehekea mwaka mmoja tangu ianzishwe

Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, leo wameungana na wafanyakazi wa kituo cha redio cha EFM cha jijini Dar es Salaam, kusherehekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

7
Zitto na Kafulila wakikata keki pamoja na wafanyakazi wa EFM

Akiongea kwenye sherehe hizo, Zitto Kabwe alisema EFM imeonesha taswira ya hali ya juu inayoakisi hali halisi ya chombo cha habari kinavyotakiwa kuwa huku Kafulila, akielezea kuguswa kwa kiasi kikubwa na vipindi mbalimbali vinavyoendeshwa na kituo hicho na kusema vinaligusa taifa.

6
Kafulila alipokua akiongea moja kwa moja kutoka katika kituo cha 93.7 EFM leo

Mkurugenzi Mtendaji wa EFM, Francis Siza, aliwataka Watanzania kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na kituo hicho ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadaye pamoja na kuliletea taifa maendeleo.

2
Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda akibadilishana mawazo na David Kafulila walipokutana katika ofisi za EFM asubuhi ya leo

Siza amesema ni muda muafaka kwa Watanzania kubadili maisha yao kuwa chanya kupitia kituo hicho na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwakuwa kipo kipo kwaajili ya Watanzania.

3
Mkuu wa Mawasiliano na mtangazaji wa kipindi cha Joto la asubuhi Dennis Ssebo akiwa na Mkurugrnzi mkuu wa EFM Francis Ciza

Naye meya wa manispaa wa Kinondoni, amesema mbali na EFM kutoa burudani pia imetoa mchango mkubwa kutatua changamoto kwa wananchi.

5
Mhariri Msaidizi wa EFM, Samira Kiango akiwa na Mkurugenzi mkuu wa EFM Francis Ciza maarufu kama DJ Majey

Pamoja na viongozi hao, hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Zantel, SUKHWINDER BAJWA.

4
Mkuu wa masoko wa Zantel, Sukhwinder Bajwa

8
General Manager wa EFM, Geofrey Ndaula akipiga stori mbili tatu na Reuben Ndege(Nchakali) pamoja Sosthenas Ambakisye(Rdj-Kamokali)

10

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents