Habari

Eminem kidogo aache hip-hop baada ya kuzomewa jukwaa


Mshindi wa tuzo za Grammy rapper Eminem hivi karibuni amezungumza kuhusiana na kutaka kuacha muziki milele baada ya kuzomewa na mashabiki jukwaani.
Slim Shady alisema kitendo hicho kilichotokea miaka 1990 kilimuumiza kiasi cha kufikiria mara mbili kama muziki ndo utakaokuwa maisha yake ama afanye mambo mengine tu.
Akiongea na mtandao wa The List, Eminem alisema “Mara ya kwanza narap mbele ya watu kwenye klabu nilizomewa. And it was very traumatic for me. I just remember it being so f***ing traumatic, and I think I went home and I was like, man, I quit. “And you know a week later, a day later, an hour later I got the urge, and I was like, I gotta get up, I gotta do it again.”
Em aliendelea kueleza jinsi hip-hop ilivyomsaidia kumpa maisha ya maana aliyonayo sasa.
Aliongeza: “naona kabisa kuwa isingekuwa rap, nisingekuwa hapa, lakini nilitoa sauti yangu, ilinipa nafasi, ilinipa nguvu, unajua nilikotokea, overdose na mambo mengine ya kipuuzi, bila rap nisingeweza kufanya chochote. Hiki ndio kitu pekee ambacho nahisi ninacho na kuweza kukifanya vyema, kama nisingekuwa na hiki sidhani kama ningefanya kitu kingine tena labda tu kucheza basketball.”
Mapema wiki hii (August 1), Eminem alikuwa mwanamuziki wa kwanza kuwa na mashabiki milioni 60 kwenye mtandao wa Facebook, na kuwashinda Lady Gaga na Rihanna kwenye rekodi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents