Habari

Equator SumaJKT waanza kuunda matrekta

Kampuni ya Equator SumaJKT kwa kushirikiana na Kampuni ya Dong Feng ya nchini China imeanza kuunda matrekta hapa nchini Tanzania na kuyauza kwa bei nafuu kwa watanzania wa kipato cha chini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Robert Mangazeni akijaribu kuendesha trekta hizo

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Robert Mangazeni, alisema kiwanda hicho kimekuwa kikipokea vifaa mbalimbali kutoka Kampuni ya Dong Feng ya China na kupitia vijana wa kitanzania ambao walipatiwa mafunzo kutoka nchini humo  kuvionganisha na kuwa matrekta.

“Kampuni ya Equator SumaJKT kwa sasa tumeanza kazi na kauli ya Rais wetu John Pombe Magufuli katika dhima yake ya Tanzania ya Viwanda, sisi tayari tumeanza kufanikisha hilo kwa vitendo na sasa tayari tuna matrekta yetu ambayo yanaundwa hapa nchini tukishirikiana na kampuni ya Dong Feng. Vijana wetu watano walipokea mafunzo na kampuni hiyo ya China na sasa wameiva wameweza kuonganisha matrekta hpana nchini na kuweza kutembea ambapo kwa siku tunaweza kuunda matreka 8,” alisema Mangazeni.

“Hawa vijana watano unaowaona, wamepatiwa mafunzo na kila mmoja tunataka atoe mafunzo kwa vijana 10, kwa maana hiyo tutakuwa na vijana 100 ambao tayari wana mafunzo na ujuzi wa kutengeneza haya matrekta, tunaweza kuwaajiri hapa na katika viwanda vyetu vingine lakini pia wanaweza kuajiriwa na kampuni mbalimbali ambazo zinatengeneza matrekta ya aina hii,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Mangazeni amezitaka kampuni mbalimbali za hapa nchini Tanzania kuanza kutengeneza vipuli vya matrekta hayo ili na wao waache kuagiza nje ya nchi.

“Kuna fursa ambazo sisi tumezizalisha, kwa sasa tunayatangazia makampuni kuanza kuteneza vipuli mbalimbia vya matrekta haya kwa sababu ni vitu ambavyo sisi tutavihitaji na hapa tunaweza kuvifanya, kwa mfano kutengeneza rejeta, nati pamoja na vifaa vingine ambayo tunavihitaji,” alisema Mangazeni.

Vijana wakiunganisha trekta

Kwa upande wa Afisa Ufundi na Mtaalamu wa Vipuli wa kampuni hiyo, Meja Mstaafu Zabron Modest amesema ujio wa kampuni hiyo ya kuonganisha matrekta nchini Tanzania itapunguza gharama za manunuzi kwa watanzania tofauti na kununua nje ya nchi.

“Kwa sasa hivi tumepata hizo trekta, zina uwezo mkubwa sana katika kazi, pia ni trekta ambazo zinaenda na wakati tofauti na zile za zamani. Lakini kikubwa zaidi ni bei, bei yake ni ndogo sana tofauti na zile ambazo zinaagizwa toka nje moja kwa moja,” alisema Modest.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents