Habari

Esther Wahome awa Mrs Universe Kenya


Muimbaji wa Gospel wa Kenya aliyewahi kutamba na wimbo uitwao ‘Kuna Dawa’ Esther Wahome jumamosi iliyopita alivikwa taji la Mrs Universe – Kenya, kwenye hafla iliyofanyika HiltonHotel, Nairobi.
Mrs Universe ni shindano lililoanzishwa mahsusi kwaajili ya wanawake ‘walioolewa tayari’ na sio kwaajili ya urembo tu bali linalenga kuyaangaza maisha ya wanawake wenye heshima.
Wahome ambaye ni mama wa watoto watatu, ataiwakilisha Kenya kwenye shindano la Mrs Universe August 13, 2012.
Shindano hilo litafanyika nchini Urusi.
Kenya ni miongoni mwa nchi chache zitakazoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho.
Tofauti na Miss World, ambayo huhusisha karibu kila nchini duniani, Mrs Universe ina washiriki chini ya nchi 50.
Kama Tanzania ingekuwa na mwakilishi, unadhani ni nani angefaa kutuwakilisha? Christina Shusho?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents