Habari

Esther Wassira aipa shavu albam ya Mansu Li

Pamoja na kuonesha uwezo mkubwa kwenye siasa, msanii na na wakili wa kujitegemea nchini Tanzania, Esther Wassira haoneshi dalili za kuachana na muziki.

Wakili huyo ameamua kumpa support rapper Mansu Li kwa kufanya kolabo kwenye wimbo uliopo kwenye albam yake ya kwanza iitwayo ‘Kina Kirefu.

Albam hiyo inatarajiwa kuingia mtaani wiki hii ikiwa chini ya usimamizi wake mwenyewe na kampuni ya Tamaduni Muzik.

Mansu Li ambaye anamfil sana Esther kwa uimbaji wake ameiambia eNewz ya EATV kuwa uhusiano wake na Esther ni wa muda mrefu kwani ni rafiki yake wa karibu hivyo haikusumbua kumpata na kuingia.

Esther Wassira

‘Kina Kirefu Iitakywa na nyimbo 20 huku akiwashirikisha wasanii wengine wakiwemo Banana Zorro, Godzilla, Chege, Jaymoe, Makamua, Joseline na Langa.

Esther Wassira ni mwanadada pekee katika albamu hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents