Burudani

Exclusive Audio: Mwana FA akielezea kwanini alikuja na wazo la show ya ‘The Finest’

Tarehe 31 May, Mwana FA atakuwa na show yake kubwa aliyoipa jina ‘The Finest’ ambapo itamuonesha hitmaker huyo akitumbuiza live na bendi ya Kilimanjaro aka Wananjenje.

70baae78c44b11e2899a22000a9f4dc8_7

“Tulipoanza kupanga kufanya mazoezi kwa tukio hili kubwa mwezi August 2012, hakuna mtu kati yetu aliyefikiri kuwa kweli tutakuja kufanikiwa live concert ya aina yake Tanzania,” anasema FA ambaye show yake hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.

“Muda wote tuliokuwa tukifanya mazoezi na Kilimanjaro Band, nimekuwa nikijituma sana kuboresha muziki wangu na moja ya matokeo yake ni hit single mpya niliyoiachia siku za hivi karibuni, ‘Kama Zamani’. Nafanya kazi kuupa uhai muziki na hiyo ndio kazi yangu.”

Kwa mujibu wa Mwana FA, The Finest ni mchanganyiko wa vizazi viwili tofauti vya muziki vinavyokutana pamoja kutengeneza kitu kikubwa. Kwanza ni yeye Mwana FA ambaye amekuwa balozi wa Bongo Flava kwa miaka 12 na kujitengenezea mashabiki lukuki na heshima kutoka pia kwa makampuni na wasanii wenzake. Pili ni Kilimanjaro Band; bendi inayoheshimika zaidi Tanzania. Pia The Finest itahusisha wasanii wengine waalikwa watakaotangazwa hivi karibuni.

The Finest itaonesha sanaa ya usimulizi wa story kupitia muziki ambapo Mwana FA atakuwa akisimulia maisha yake na muziki anaoufanya kulinganisha na maisha ya Mtanzania wa kawaida anayepambana kupata maisha mazuri kwa njia halali. Mwana FA anasema The Finest sio tu show ya muziki bali movement ambayo itaenda kusogeza mbele hadhi ya muziki wa Tanzania.

Msikilize zaidi hapa;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents