Burudani

Exclusive: Camp Mulla ft. Wizkid – Prices (Monster Hit)

Collabo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ya kundi lililojichukulia sifa kwa kuwakilisha Kenya na style yao 254, Camp Mulla na msanii ambaye kwa sasa Akon anakumbali zaidi barani Africa, Wizkid wa Nigeria, imetoka! What more can we say!! Ofcourse, as we expected, it’s a hit!!

Ngoma inaanza kama kawaida ya outro yao, ‘think you can handle Camp Mulla?” Kisha wameamua kumpa mgeni wao (Wizkid) nafasi ya kwanza kwa kufungua verse. Wizkid unaweza kumsahau kidogo humu! Amepunguza zile swagga za kinaijeria kidogo na kuonesha uwezo wake katika style ya RNB! Huo ni uamuzi mzuri sana kumwacha aanze mwanzo kwakuwa wengi walitaka kumsikia angefit vipi kwenye 254 hivyo jibu wamelipata mapema tu.

Wizkid

Baada ya Wizkid amefuata Shappa Man ambaye kama kawaida amenail mdundo! Kisha chorus inafuata ambapo Wizkid anasikika akisema, ” We don’t even ask for prices no more” halafu anasikika mcamp mulla mmoja akisema maneno ambayo kwa Kiswahili anamaanisha kuwa anapokwenda kwenye maduka kununua kitu hana haja ya kuuliza tena bei! Hakuna tena zile za ‘Hiki kiatu ni bei gani? Wakati chorus inaendelea anadakia first lady wao Miss Karun akisema, “Cause we bawl, we top charts, we young catz, we work hard!!

Miss Karun anaitoa ile sauti yake tamu ambayo haiendani na umbo na umri wake! Sauti tamu inayoweza kumtoa nyoka pangoni. Utemi dhidi ya beat unaendelea kwa member wengine wa kundi hili.

Hii ngoma ni kali na kwa video zao, huenda ikawapeleka mbali zaidi ya hapo walipo sasa.
Nice collaboration na Bongo inaipa nyota 5!

Isikilize hapa:
http://soundcloud.com/campmulla254low/camp-mulla-prices-ft-wiz-kid

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents