Habari

Exclusive Video: Angel akanusha Watanzania kuonewa kwenye TPF6, akiri hakufanya vizuri licha ya kuwa na uwezo

Aliyekuwa mmoja wa wawakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Tusker Project Fame msimu wa 6, Angella Karashani amekiri kuwa aliimba chini ya kiwango kiasi cha kumfanya atoke mapema.

http://www.youtube.com/watch?v=6H12qesh20I&feature=youtu.be

Akiongea kwenye interview exclusive na Bongo5, Angel amesema kwa uwezo wake alitegemea kuwa angefanikiwa kufika hadi Top 5.

“Personally nahisi sikufanya vizuri sana kutokana na kwamba najua uwezo wangu. I think pressure na baadhi ya vitu vingine kidogo sikuwezA kuperform to the best of my ability,” amesema Angel.

Angel ameongeza kuwa uoga na ugeni wa stage ndio uliomponza hadi kushindwa kufanya vizuri kwenye shindano hilo NA hatimaye kutolewa Jumamosi iliyopita.

“Sijawahi kupata nafasi ya kuperform kwenye jukwaa lenye watu wengi, sio tu wale watu wapo mle ndani, ile kufikiria kwamba you are live on television, una watu zaidi ya milioni 10 wanakuangalia, kila mtu anasubiri kuangalia utateleza wapi, utaharibu nini. Kwangu hiyo ndio ilikuwa pressure kubwa ile kusema ‘will I deliver? Kwahiyo ukianza tu na ukiona tu ‘hapa sio kama nilivyoplan kuanza, Maybe unavyoanza kuimba, ukishafika katikati ya nyimbo and then zile kelele sio kama za mtu aliyepita ama za mtu mwingine au sio kama ulizotarajia wewe kuzipata kidogo inakuwa discouraging.”

Hata hivyo Angel amekanusha madai kuwa washiriki wa Tanzania wamekuwa wakionewa kwenye shindano hilo.

“Siwezi kusema kwamba Watanzania tunaonewa. Wakenya wako juu sababu wanashirikiana sana. ni kitu ambacho bahati mbaya ama nzuri Watanzania hatuna, hatuna ile support ya home. Kwasababu hata mimi nilivyokuja nimepitia social networks na nadhani theluthi ya Watanzania wanasupport watu wengine zaidi ya Hisia,” amesisitiza Angel.

Ametoa mfano wa Kenya kuwa hata kama wana mshiriki ambaye hana nafasi ya kushinda, wamekuwa na umoja na kuwapigia zaidi kura.

“Siwezi kuweka kwenye maneno kwamba Watanzania tunaonewa kwasababu mimi sijaiona hiyo. Hata nilipokuwa ndani ya academy na malezi yetu, sikuona mtu yoyote ambaye kapewa kipaumbele, kila mtu alikuwa sawa.”

Katika hatua nyingine, Angel amesema kinachofuata baada ya kutoka kwenye mashindano hayo, ni kuachia wimbo mpya na kwenda kusomea muziki, Sauti Academy ya nchini Kenya.

“Nategemea kutoa single, bado sijajua ni ipi na sijajua ni lini lakini nitawaambia. Pia naplan kwenye kusomea muziki kiprofessional zaidi mwakani,” amesema muimbaji huyo.

Amesema kushiriki kwenye TPF6 kumemfanya aweze kujifahamu zaidi ikiwa pamoja na kujigundua kuwa yeye ni muoga na hivyo kwenda shule ni muhimu ili kuondoa kasoro hizo.

“Nimegundua kuwa mimi ni muoga wa stage, kitu ambacho nilikuwa sijui. Nashukuru sana TPF imenifanya nigundue hicho kitu hadi nimefikia hatua ya kwenda kusoma kwenye shule ambayo itaniexpose kama performer.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents