Habari

Exclusive Video: B12 aelezea jinsi nguo za Born 2 Shine zinavyokua brand kubwa Afrika Mashariki

Brand ya Born 2 Shine inaendelea kuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki baada ya t-shirts zake kuvaliwa na mastaa kibao wa Tanzania. T-shirts hizo tayari zimeonekana kuvaliwa na AY kwenye video yake Money na video mpya ya Diamond, Number 1 ambazo zote zilifanyika nchini Afrika Kusini.

Alhamis hii wakati wa uzinduzi wa video mpya ya Diamond kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Number 1, tumepiga story na mhasisi wa brand hiyo, Hamis Mandi aka B12, ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi maarufu cha XXL cha Clouds FM kutaka kujua safari ya brand hiyo hadi muda huu.

“Mwanzoni ilikuwa naadvertise tu duka kawaida. Kwahiyo nikawa nimetengeneza t-shirts zangu tu kadhaa kwaajili ya kuitengeneza brand ya duka langu,”anasema B12.

“Siku moja Shetta akaja pale akaniambia ‘hizo t-shirts za Born 2 Shine kali naomba nikavae kwenye show yangu Billicanas’ so nikampa t-shirts kama tano hivi akavaa yeye na dancers wake. Baada ya ile show ndio nikagundua kumbe hiki kitu kama watu wanakihitaji hivi, kila mtu akawa anaulizia, ‘ntapata wapi hizi t-shirts’ nawaambia zinapatikana Born 2 Shine, duka kipindi hicho ndo jipya halina hata kiki, so nikashangaa kila siku watu wanakuja kuulizia zile t-shirt, nikaona kumbe kuna fursa huku pia!”

B12 anasema katika kuitangaza zaidi brand yake, amekuwa akiwashirikisha wasanii wa muziki na filamu ambao kwa kiasi kikubwa wameisaidia brand hiyo kubwa zaidi. Miongoni mwa wasanii walioitangaza sana brand hiyo ni AY na Diamond ambao wote wamezitumia t-shirts zake kwenye video zao za kimataifa..

“AY mimi ndio nilimuombna,” anasema. “Nilimuomba AY ‘kama kuna uwezekano wa kuvaa t-shirt yangu kwenye video yako, nitaappreciate, akaniambia ‘nitengenezee yangu special. Kama umeona ile t-shirt, ni special ile, ina rangi nyingi sana. Gharama ya kutengeneza ile t-shirt ni kama elfu 32 hivi, gharama yake tu ya kuprint ile, bila gharama ya t-shirt yenyewe, so ni expensive kidogo nikaona sio kesi sababu jamaa ataenda kunitangaza,” amesema.

“Lakini kwa Diamond, nikikuambia hiyo t-shirt Diamond ameinunua lini huwezi kuamini. Aliinunua Mbeya kwenye Fiesta ya mwaka jana, akaniambia nimuuzie baadhi ya t-shirt za Born 2 Shine, nikamuuzia, kumbe hakuwahi kuivaa sehemu yoyote. Siku ananitumia picha ananiambia ‘surprise’ sasa mimi sikuelewa anafanya nini, akaniambia ‘itatokea kwenye video yangu mpya’. Nilihisi kama amenipa blessing za hatari sana so inanidi kunipa nguvu.”

B-Dozen amesema mipango aliyonayo kuhusu brand hiyo na kabla mwaka huu haujaisha amesema anatarajia kufanya mapinduzi makubwa kwenye masuala ya mavazi ambapo si kwa vijana tu bali anataka iwafikie watu wazima pia.

“Kwasababu tumeangalia ni jinsi gani tunaweza tukaipenyeza ile Born 2 Shine hata kwa wazee kwenye polo shirts kali sana lakini inakuwa ni brand ya Born 2 Shine. This time around tunakuja na logo ya Born 2 Shine. Tukishaintroduce hiyo logo hapo sasa nafikiri hapa mjini kiukweli tutakimbizana kidogo na malengo yetu ni kuipeleka international sababu mtu akivaa t-shirt ya Born 2 Shine unaulizwa especially ukiwa nje ya nchi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents