Habari

Fabolous: Mama yangu hajafa



Rapper wa Brooklyn Fabolous amekanusha ripoti zilizoandikwa na mtandao namba moja kwa udaku nchini Marekani wa MediaTakeOut kuwa mama yake mzazi amefariki dunia.
Fab aliamua kuutumia mtandao wa Twitter kukanusha ripoti hizo mbaya kumhusu mama yake.
“ FYI, my MOM did not die. Keep seeing tweets sayin’ RIP to my mom. Think some people misunderstood my Instagram pic’s caption,” rapper huyo aliandika.
Maelezo ya chini (caption) ya picha hiyo yanasomeka, “She held on as long as she could … my mom,” na kumuonesha rapper huyo wakati mtoto akiwa amebebwa na mama yake.
Kutokana na picha hiyo pamoja na maelezo hayo, MTO ilihisi kuwa huenda mama yake amefariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents