Burudani

Familia ya Sharo Milionea kuachia filamu ya maisha yake (Sharo)

Familia ya marehemu Sharo milionea inatarajia kuachia filamu itakayooenesha maisha yake tangu anazaliwa kijijini kwao huko Muheza mkoani Tanga pamoja hustle zake wakati ameingia jijini Dar es Salaam.

sharomilionea

Akizungumza na Clouds FM mmoja wanafamilia ya Sharo amesema filamu hiyo ya maisha ya marehemu Sharo itachezwa na waigizaji mbalimbali wakiwemo King Majuto, Asha Boko na baadhi ya ndugu zake akiwemo mama yake.

“Kwa sasa hivi mipango wa familia tumeanza kuandaa documentary ya marehemu Sharo. Baadhi ya picha za wazi na picha nyingine baadhi ya scenes zitapigwa. Halafu kuna filamu ambayo dada yangu mimi ameicheza na mimi nyenyewe ila hiyo tutaiweka pending kwanza. Tutaanza na filamu ya Sharo. Ni story yake binafsi ‘Sharo’ toka anatoka nyumbani kuhustle kuhusu muziki na mambo yake ya sanaa haya na maisha binafsi akiwa Dar es Salaam,” alisema ndugu huo.

Sharo Milionea alifariki dunia kwa ajali November mwaka juzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents