Habari

Faru mweupe ‘Sudan’ aliyekuwa amesalia duniani amekufa

Dunia imepokea kwa mshituko kifo cha faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani.

Faru huyo akiwa katika hifadhi hiyo.

Faru huyo amekufa akiwa na miaka 45 akiwa kwenye hifadhi ya shirika la Ol Pejeta lililopo Nanyuki nchini Kenya.

Kwa mujibu wa shirika hilo, Sudan alikuwa akitibiwa kwa muda matatizo na magonjwa ambayo yalitokana na kuzeeka kwake.

Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.

Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

“Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana,” Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.

“Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake.”

Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.

Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove nchini Jamhuri ya Czech miaka ya 1970.

Mwaka 2009, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta katika jimbo la Laikipia.

Alichangia kuendeleza faru wa aina yake kwa kutungisha mimba faru wengine na kuchangia kuzaliwa kwa faru wengine wawili wa aina yake ambao sasa ndio pekee waliosalia hai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents