Burudani

Fella aeleza jinsi Sh 50 milioni za Kayumba wa BSS zilivyotumika mpaka kwisha

Meneja wa mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma, Saidi Fella amefunguka juu ya kukata kwa mkwanja wa msanii huyo kabla ya mjengo wake kukamilika.
Kayumba SA

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Fella alisema kuwa mkwanja wa msanii huyo mpaka sasa umekata kutokana na matumizi mengine ambayo yalikuwa ni ya muhimu hivyo atachelewa kuwaonesha mashabiki zake kama ambavyo alikuwa amewaahidi hapo awali.

“Pesa yake ilitumika kwa ajili ya kutengeneza video, kununulia gari pamoja na kujenga nyumba yake hadi pale ilipofikia, ila kwa sasa nategemea Kayumba aanze kupige shoo ili aweze kuingiza pesa itakayosaidia kumalizia kujenga nyumba yake,” alisema Fella.

Kayumba aliwaahidi mashabiki zake kuwa atawaonesha mjengo wake anaoujenga ikiwa ni sehemu ya matumizi ya shilingi milioni 50 za ushindi wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents