Femi Kuti kuwa jaji wa Nigerian Idol

Baada ya msimu wa pili wa mafanikio wa shindano la Nigerian Idol, waandaaji wanajipanga tena kufanya mambo makubwa kwa msimu wa tatu na safari hii kitu cha kusisimua zaidi kikiwa ni kuingia kwa mwanamuziki mashuhuri, Femi Kuti katika dawati la majaji wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa meneja wa shindano hilo Tiwa Medubi, kuingia kwa Kuti safari hii umeazimia kuleta mabadiliko na ladha tofauti tofauti ili kuyaongezea mvuto zaidi.

Akizungumzia uteuzi wake huo, Kuti amesema kuwa anajisikia heshima kuwa sehemu ya Nigerian Idol, shindano ambalo linazunguka kusaka vipaji mbalimbali vya muziki kitu ambacho anakipenda na ni sehemu kubwa ya maisha yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents