Burudani

Fid Style Friday kuruka kwa mara ya kwanza July 20


Hatimaye wapenzi wa Hip Hop nchini wana uhakika wa kuitazama show ya mc mkali nchini Tanzania, Fareed Kubanda aka Fid Q, kuanzia ijumaa hii kupitia EATV.
Show hiyo ambayo awali ilikuwa ikionekana kwa njia ya mtandao zaidi sasa itawafikia watanzania wengi ambao walikuwa hawawezi kuiona kwenye internet.
Kabla ya uamuzi huo wa kuitafutia kituo cha runinga show hiyo, mashabiki wengi wa Fid Q walimshauri kuangalia uwezekano huo kwakuwa alikuwa hawatendei haki wale wasio na uwezo wa kutumia internet.
Show hiyo ya Fid Style Friday humhusisha Fid kama host wake na ambaye huzungumza na wasanii wenzie wa hip hop ambapo mara nyingi wasanii hao huwekea beat na kuanza kuchana mistari.
Mpaka inasitishwa kutolewa kwenye internet, Fid alikuwa ameshawatembelea wasanii kama One the Incredible, Nikki Mbishi, Stereo,Langa, Zaiid na wengine.
Kabla ya kuwa maarufu kwenye muziki wa hip hop, Fid Q alikuwa na ndoto za kuja kuwa mtangazaji na kuna wakati alitaka kuomba nafasi ya kutangaza kwenye kituo cha radio cha Kiss FM cha jijini Mwanza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents