Burudani

Filamu ya ‘Straight Outta Compton’ yaingiza dola milioni 56.1 katika wiki yake ya kwanza

Filamu ya ‘Straight Outta Compton’ imeingiza dola milioni 56.1 na kukamata nafasi ya kwanza kwenye box office nchini Marekani.

soc-nwa

Filamu hiyo iliyoongozwa na F. Gary Gray inaangaza maisha ya kundi la zamani la Hip Hop la N.W.A lililoundwa na wasanii kama Dr Dre, Ice Cube, Eazy E na wengine.

Filamu hiyo imeweka rekodi ya kuwa filamu inayotazamwa na watu wazima tu yaani R-rated film na kuivunja rekodi ya filamu ya American Pie 2 ya mwaka 2001 iliyoingiza dola milioni 45.1.

Imezizidi pia filamu za historia ya muziki zikiwemo Walk the Line ($22.3 million) ya mwaka 2005 na 8 Mile ya Eminem ($51.2 million) ya mwaka 2002.

Filamu hiyo ilitengenezwa kwa bajeti ya dola milioni 29.

Wakati huo huo album ya Compton: A Soundtrack ya Dr. Dre nayo iliuza kopi 300,000 katika wiki yake ya kwanza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents