Burudani

G-Nako: Upendo ndio siri ya kubwa ya Weusi kuendelea kuwa pamoja

G-Nako amedai kuwa siri kubwa ya kwanini kundi la Weusi limeendelea kuwa pamoja na kufanya muziki mzuri ni upendo kati yao.

10945342_354987064695960_1378053063_n

Weusi ndio kundi la hip hop imara zaidi kwa sasa nchini na linaundwa na wasanii watano japo wanaosikika zaidi ni G-Nako, Joh Makini na Nick wa Pili. Wengine ni pamoja na Lord Eyez na Bonta.

“Sisi cha kwanza ambacho huwa tunasimamia nacho ni upendo,” G-Nako alikiambia kipindi cha Dala Dala Beat cha Magic FM.

“Upendo unakuja kabla ya kila kitu. Kwahiyo tayari upendo umeshatuweka pamoja na vingine vinafuatia.”

Katika hatua nyingine G-Nako amesema bado hawana mpango wa kuongeza wasanii wengine kwenye kundi/kampuni yao lakini wanakaribishwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye kampuni yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents