Habari

Gari la ziara la 2 Chainz lakamatwa likiwa na silaha na madawa

Pistol mbili, shotgun moja na dawa za kupunguza maumivu vilipatikana kwenye basi la tour la 2 Chainz mwezi uliopita alipokamatwa na watu wengine 10, kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani zilizowasilishwa jana.

article-2410624-1B9BDA63000005DC-380_634x825

Rapper huyo mwenye miaka 35, ambaye jina lake halisi ni Tauheed Epps, alikamatwa August 22 kwenye jiji la Oklahoma City baada ya polisi kusimamisha basi hilo.

Kwenye ukaguzi huo polisi walikamata pia madawa ya hydrocodone na Flexeril ambayo hayakuwa yameelekezwa na daktari. Flexeril hutumika kupoza misuli na hydrocodone hupunguza maumivu. Maofisa pia walikamata mabaki ya bangi na karatasi za kusokotea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents