BurudaniUncategorized

Goodluck Gozbert (Lollipop): Nilishamsamehe Abby Dady

Prodyuza Goodluck Gozbert maarufu kama Lollipop amesema ameshamsamehe prodyuza mwenzake Abby Dady ambaye alimtuhumu kwa kuiba wimbo na kwenda kumpatia Ommy Dimpoz.

Licha ya msamaha huo, Lollipop ameeleza kuwa kiustaarabu au kiutaratibu inapotokea mtu kaibiwa wimbo anatakiwa kumtafuta muhusika na kumpatia taarifa lakini yeye hakuwahi kupatiwa taarifa zaidi ya kuona kwenye mitandao.

“Nilisikia taarifa kwenye mitandao mimi nikakaa kimya, baada ya muda nikaona amemuomba radhi Ommy Dimpoz kwa kusema hakufanya kitu poa, kwa hiyo mimi binafsi nilishamsamehe,” ameiambia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.

“Kuhusu suala la wimbo kuibiwa anafahamu ukweli, historia haijwahi kudanganya halafu kitu kilichonisikitisha anasema wimbo umeibiwa kutoka kwa msanii chipukizi wakati ni watu ambao nimekuwa nikifanya nao kazi kwa kuwasaidia,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents