Michezo

Guardiola aeleza alivyompania Maurizio Sarri “walitufunga kwao na wakati yupo Napoli pia, nilijua alichotaka kutufanyia watu hawajui tu”

Kocha wa klabu ya Manchester City Mhispania Pep Guardiola amefunguka baada ya mchezo wake wa jana dhidi ya Chelsea ambapo Manchester City walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6 kwa 0.

Mhispania huyo ameongea baada ya mchezo huo na kueleza ni jinsi gani alivyojiandaa kumuangamiza mwenzake wa Chelsea Maurizio Sarri.

Guardiola Alipoulizwa ikiwa hakuwa na huruma na Sarri, Guardiola alisema: “Ndio bila shaka, najua hasa alichotaka kufanya. Nadhani nawajua sana aina hii ya watu ingawa amesaidia kufanya soka yetu Uinereza kuwa bora zaidi. “Walitufuga Stamford Bridge na pia dhidi ya Napoli msimu uliopita licha ya kuwa Wakati huo wa michezo hiyo, walikuwa bora kuliko sisi”

“Watu hawaelewi jinsi ilivyo vigumu kumfunga” Nilisema mara nyingi, mwaka wangu wa kwanza ulikuwa mgumu pia. Wakati fulani tulicheza vizuri lakini si mara kwa mara. “Watu wanatarajia ‘Sawa, meneja anapofika, hununua wachezaji na huja mara moja moja na matokeo mazuri inahitaji muda kidogo Itategemea imani kutoka kwa wamiliki, watu wanaohusika, wanahitaji kweli kuamini hivyo. “Sababu kuu niliyoamua kuja Manchester City ni kwa sababu wakubwa wangu, mwenyekiti hasa, sikuhitaji kumshawishi Yeye ananijua vilivyo”

Guardiola aliongeza kuhusu ugumu wa kufanya kazi kama kocha na alisema ” Mambo yanapokuwa magumu huwa natafuta njia ya kuyatatua na huwa niko vizuri ninaposhinda watu wanajua hilo ila ninapopoteza mambo hubadilika”

Wakati anaelezea kipigo dhidi ya Chelsea na kutokusalimiana na Sarri alisema “Nilizungumza na msaidizi wa Chelsea Gianfranco Zola,” Guardiola aliongeza. “Maurizio Sarri hakuona mimi nina uhusiano mzuri pamoja naye kwa hiyo sio shida kabisa.”

Manchester City sasa wapo kileleni na alama 65 sawa na Liverpool ingawa City wako mbele kwa zaidi ya mchezo mmoja na wanaidadi kubwa ya magoli.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents