Happy Birthday Hamis Mwinjuma aka Mwana FA (soma historia yake fupi)

Leo ni siku ya kuzaliwa ya rapper Hamis Corlone Mwinjuma aka Mwana FA. Ni rapper anayeaminika kuwa miongoni mwa waandishi bora kabisa wa mashairi ya Hip Hop kuwahi kutokea katika muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.

IMG_3768-640x427

Aliamua kuingia kwenye muziki baada ya kuvutiwa na binamu zake China Black na Kasir waliokuwa na kundi liitwalo Quite Gangsters Chronic(QGC). Akiwa Muheza mkoani Tanga anakotokea, Mwana Falsafa alianzisha kundi liitwalo Black Skin akiwa na washkaji zake wa shule Robby Ras na Getherics mwaka 1995.

Mwaka 1996 walikamata nafasi ya tatu kwenye shindano la michano la mkoa wa Tanga. Mwaka 1998 alikwenda Dar es Salaam kusoma high school na kufanikiwa kutoa ngoma iliyompa umaarufu ‘Ingekuwa Vipi?’ akiwa na Jay Mo na pia ‘Mabinti’ ambayo ilitayarishwa na Bonny Luv.

Mwaka 2003, ngoma yake ‘Alikufa Kwa Ngoma’ – ilimpa tuzo kama wimbo bora wa Hip Hop wa mwaka kwenye Kili Music Awards. Mwana FA aliendeleza utemi kwa kuachia hits kibao kama Unanitega, ‘Hawajui’ feat. Lady Jaydee, Habari Ndio Hiyo akiwa AY, Bado Nipo Nipo, Unajijua Unanisikia, Yalaiti na ngoma ya hivi karibuni Ameen.

Mwaka huu anasubiriwa kwa hamu kuachia ngoma yake mpya iitwayo Kama Zamani aliyowashirikisha Njenje.

Pamoja na kufanya muziki, Mwana FA aliamua kwenda nchini Uingereza kuongeza shule yake ambako alisoma shahada ya Finance katika chuo kikuu cha Coventry. Kwa sasa ameanzisha pia kampuni ya kusimamia wasanii iitwayo Lifeline Music Inc ambayo tayari ina msanii mmoja aitwaye Maua Sama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents