Michezo

Hatimaye Luis Suarez atua Barcelona kwa pauni milioni 75

Klabu ya soka ya Liverpool imekubali kumuuza mshambulizi wake Luis Suarez kwa Barcelona kwa pauni milioni 75.
article-2688777-1F9198B600000578-435_634x346

Mchezaji huyo wa Uruguay ,ambaye amepigwa marufuku ya kutocheza mpira miezi miinne baada ya kukutwa na hatia ya kumng’ata begani mchezaji mwenzake wa Italy, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao katika kombe la dunia anatarajia kusafiri kwenda Barcelona wiki ijayo kwajili ya vipimo.

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers alisema: Luis ana kipaji cha kipekee, na ninamshukuru kwa alivyotuwakilisha,
Suarez anasema kuwa yeye pamoja na familia yake, daima watakuwa mashabiki wa Liverpool.

Hatua ya Suarez kuhamia Barcelona inampeleka karibu na mkewe pamoja na familia yake.

“Ni kwa majonzi mengi nimeamua kuondoka Liverpool, kwa maisha mapya nchini Uhispania na cha mno ni kwamba nimefurahishwa sana na mashabiki. Ninatumai nyote mtaelewa uamuzi wangu. Klabu hii ilinifanyia kila nilichokitaka, lakini kucheza na kuishi uhispania, ilikuwa ndoto yangu kubwa. Muda huu uko sawa sana kwangu. Ninamtakia Brendan Rodgers na kikosi chake kila la heri na mustabali mwema. Klabu hiyo iko chini ya usimamizi mzuri na pia natumai watafanikiwa msimu ujao.” Alisema Luis Suarez

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents