Habari

Hatukamati mwanasiasa tu – IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema jeshi hilo halina lengo la kuwakamata wanasiasa kwa kuwaonea ila linawakamata watuhumiwa kutokana na makosa mbalimbali na endapo ushahidi utaonyesha hawahusiki na jambo walilokamatiwa wataachiwa huru kwa mujibu wa kanuni na sheria.

IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Tanga alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano wake alioufanya na askari wa jeshi hilo mkoani humo.

“Sisi tunakamata mtuhumiwa, tunakamata mtu ambae tunaamini kwamba amefanya kosa la jinai hatukamati mwanasiasa tu hapana tunakamata mtuhumiwa ambaye tunajua amefanya kosa kwahiyo tukipeleleza tukibaini kuwa tuhuma hizo si za kweli tuna muachia tukiona tuhuma hizo za kweli tunampeleka Mahakamani,” alisema IGP Sirro.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents