Aisee DSTV!
SwahiliFix

Haya ndio yaliyojiri mahakamani kwenye kesi inayomkabili Mwandishi wa Habari Erick Kabendera

Mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Erick Kabendera (39), anayekabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha fedha zaidi ya Tsh milioni 173, Leo Agosti 19, 2019 amerudishwa rumande hadi Agosti 30 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Shauri hilo limetajwa leo Jumatatu Agosti 19, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Mmbando kwa sababu Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile anayesikiliza kesi hiyo kupata udhuru.

Katika shauri hilo, imeelezwa kuwa Kabendera na wenzake ambao hawapo mahakamani alitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha na kukwepa kodi ya Tsh milioni 173 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) .

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW