Habari

Hii ndiyo kauli ya kwanza ya Zitto Kabwe baada ya uteuzi wa Anna Mghwira

Baada ya uteuzi wa Rais Magufuli jana wa Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghwira kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kulikuwa na mijadala mizito mitandaoni na hata kwenye vyombo vya habari juu ya uteuzi huo huku wengi wakimtaka Mbunge pekee wa chama hicho, Zitto Kabwe atolee ufafanuzi juu uteuzi huo hatimae leo ametoa kauli yake ya kwanza kuhusu uteuzi huo.

Tokeo la picha la zitto Kabwe na anna mghwira
Zitto Kabwe akiteta jambo na Mama Anna Mghwira

Zitto Kabwe amesema amezipokea taarifa hizo kutoka mitandaoni na kwenye vyombo vya habari lakini bado Chama cha ACT wazalendo hakijafanya mawasiliano na Mghwira anmbaye yupo nje ya nchi mpaka atakaporejea ndipo chama kitatoa msimamo wake juu ya uteuzi huo.

Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.“ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hata hivyo Zitto Kabwe amewataka Wanachama wa chama cha ACT wazalendo luwa watulivu kwa kipindi hiki mpaka hapo taarifa rasmi itakapotolewa pindi atakaporejea nchini.

Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.“ameandika Zitto Kabwe.

https://youtu.be/zMmDnTvcX7E

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents