Habari

Hiki ndio kiasi kilichovunwa na Jeshi la Polisi kupitia makosa ya usalama barabarani kwa siku 10 (+video)

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani limeingiza kiasi cha tsh bilioni 1 kwa faini za makosa ya Usalama Barabarani kuanzia tarehe 24 Novemba 2017 hadi tarehe 04 Desemba 2017.

Kamanda Lazaro Mambosasa

Akiongeza na Waandishi wa Habari, Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa amesema wamekamata magari 32,471, Pikipiki 1,145, Daladala 10,752, Magari mengine (binafsi na malori) 21,719 na Bodaboda 55 wamefikishwa Mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmet ambapo kwa ujumla wamefanikiwa kukusanya tozo la kiasi cha tsh  1,007,610,000 /=.

Kwa upande mwingine Kamanda Mambosasa amewaasa wananchi kutumia namba 41.59.7.174/tms kwa simu zao za mikonononi zenye uwezo wa internet kwa kutumia Browser ya google kwa maulizo ya faini zilizoandikwa kwa mashine za kielektroniki Traffic Management Systems (TMS) huku  akiwataka madereva kulipa faini ndani ya muda wa siku saba (7) ili kuepukana na usumbufu wa kukamatwa pamoja na ongezeko la tozo za faini.

Tazama video ya Kamanda Mambosasa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents