Habari

Mtanzania afariki ndani ya ndege akisafirisha dawa za kulevya

Mtanzania aliyekuwa anasafirisha madawa ya kulevya kupeleka nchini China amefariki kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia baada ya kuzidiwa na dawa hizo.

Rogers Sianga

Akithibitisha taarifa hizo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), Rogers Sianga amesema amepokea taarifa hizo jana Desemba 4, 2017, ila bado wanafanya uchunguzi zaidi kujua jina lake na wapi alizitoa dawa hizo.

Ni kweli kuna Mtanzania amekutwa amekufa kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia akiwa amemeza dawa za kulevya. Tunaendelea kufuatilia kujua jina lake na amezitoa wapi hizo dawa.” amesema Sianga kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.

Kwa upande mwingine Sianga amesema Watanzania wengi wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya  wanatumika kwa kupokea mizigo hiyo na kuisafirisha kunakohitajika kitu ambacho bado serikali inapambana nacho ili kuweza kutokomeza kabisa biashara hiyo haramu..

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents