Habari

Hili ndio jiji la kifahari zaidi duniani mwaka 2017, Halitoki Marekani wala Uingereza

Kwa mujibu wa Tafiti zilizofanywa na jarida la mitindo la Zalando jiji la Paris ndio jiji la kifahari zaidi duniani kwa mwaka 2017, likichukua nafasi ya jiji la London ambayo mwaka jana 2016 lilitajwa na jarida hilo kuwa ndio jiji la kifahari.

Tokeo la picha la Paris
Paris, Ufaransa.

Kwenye orodha ya majiji 100 ya kifahari zaidi kuishi duniani nafasi ya pili imechukuliwa na jiji la London, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na jiji la Vienna mji mkuu wa Austria.

Kwenye orodha ya majiji 10 kati ya 100 yaliyotajwa na jarida hilo, Italia ndio nchi iliyotoa majiji mengi ya kifahari ikitoa majiji matatu, Ikifuatiwa na Ufaransa iliyotoa majiji mawili.Tazama orodha kamili ya majiji 20 na idadi ya kura yalizopigiwa

Kwenye orodha hiyo ya majiji kumi Marekani, Italia na Hispania zote zimeenda sawa kwa kutoa jiji moja moja kila nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents